Monday, August 18, 2014

Today's news






Posted: 17 Aug 2014 09:55 AM PDT

Posted: 17 Aug 2014 09:28 AM PDT
Mtoto wa Kitanzania, msichana Neema Steven Mtwanga, ameibuka kinara katika Mashindano ya Utunzi wa Insha katika nchi wanachama wa Jumuia ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kwa kushika nafasi ya kwanza miongoni mwa washindani 39 waliowania Tuzo ya Utunzi wa Insha hiyo kwa Mwaka 2014. 
Msichana Neema Steven Mtwanga, 16, kutoka Shule ya Sekondari ya Naboti, Mkoa wa Njombe, ametunukiwa Tuzo ya ushindi huo katika Mkutano wa 34 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa SADC ulioanza leo katika Hoteli ya Elephant Hills Resort, Victoria Falls, Zimbabwe. 
Nafasi ya pili imeshikwa na Kudzai Ncube kutoka Shule ya Sekondari ya Mazowe nchini Zimbabwe na nafasi ya tatu imeshikwa na Manxoba Msibi kutoka Shule ya Sekondari ya Etjendlovu katika Swaziland. 
Kwa ushindi huo, Neema Steven Mtwanga ambaye yuko kidato cha nne, amezawadiwa hundi ya dola za Marekani 1500 ambayo ni sawa na shilingi milioni 2.3 na amelipiwa gharama zote za kumwezesha kushiriki katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za SADC na kukabidhiwa zawadi hiyo. Aidha, Neema amepewa zawadi ya ipad kwa ajili ya matumizi yake ya teknolojia ya mawasiliano na habari. 
Mashindano hayo ya Insha ya Mwaka 2014 yalianzishwa rasmi Oktoba, 2013 ambako washindani walitakiwa kuandika Insha kuhusu mada: "Climate Change is having adverse effect on the socio-economic development in the Region. What should the Education Sector do to mitigate the impact on the youth" – Mabadiliko ya Tabia Nchi yanaathiri maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Kanda ya SADC. Nini Sekta ya Elimu ifanye kupunguza athari hizo kwa vijana? 
Insha 39 zilipokelewa kutoka nchi 13 kati ya nchi 15 wanachama wa SADC ikiwa ni Insha tatu kwa kila nchi. Insha zilipokelewa kutoka Tanzania, Angola, Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Lesotho, Malawi, Mauritius, Mozambique, Namibia, Afrika Kusini, Swaziland, Zambia na Zimbabwe. 
Majaji wa kupitia na kuamua washindi wa Insha hizo walitoka Tanzania, Zambia na Zimbabwe na walikutana mjini Gaborone, Botswana, Julai, mwaka huu kupitia Insha zote na kutoa uamuzi wa nani washindi. Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huo wa SADC umepokea kwa furaha ushindi wa msichana Neema ukieleza kuwa ushindi huo umeiletea Tanzania heshima kubwa katika eneo la SADC na nje ya eneo hilo. 
Imetolewa na; 
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, 
Ikulu – Dar es Salaam. 
17 Agosti,2014
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mwanafunzi wa kidato cha nne Neema Steven Mtwanga(16) anayesoma katika shule ya sekondari Naboti Makambako,Njombe baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika utunzi wa insha katika shindano lililoandaliwa na Jumuiya ya uchumi ya maendeleo kusini mwa Afrika(SADC).Rais Kikwete alimpongeza mwanafunzi huyo wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 34 wa wakuu wa nchi za SADC unaofanyika katika mji wa kitalii wa Victoria Falls, nchini Zimbabwe ambapo mwanafunzi huyo aliandika insha inayohusu mabadiliko ya tabia nchi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wakuu na wawakilishi wa nchi za Jumuiya ya uchumi kusini mwa Afrika SADC muda mfupi baada ya ufunguzi wa mkutano wa 34 wa jumuiya hiyo uliofanyika katika hoteli ya Elephant Hills mjini Victoria Falls Zimbabwe leo.Katikati ji mwenyeji wa Mkutano huo Rais Robert Mugabe na  Dkt Stergomena Tax [katibu mkuu wa SADC] na kwa upande wake wa kushoto ni Nkosazana Dlamini-Zuma  (Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika)
Posted: 17 Aug 2014 09:28 AM PDT

Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Rais Robert Gabriel Mugabe wa Zimbabwe akimkabidhi Bi. Sheila Hashim Mbita, binti yake Brigedia Jenerali Mstaafu Hashim Mbita Tuzo ya Juu ya Taifa la Zimbabwe ya Nishani ya Royal Order Of Mwanamutapa kwa kutambua mchango wake katika ukombozi wa Taifa la Zimbabwe na nchi nyingine kusini mwa Afrika. Rais Mugabe alikabidhi tuzo hiyo wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 34 wa wakuu wa SADC unaofanyika katika mji wa kitalii wa Victoria Falls, nchini Zimbabwe. Picha na Fred Maro
---------------------------
Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imeishukuru na kuipongeza tena Tanzania kwa mchango wake mkubwa na wa hali na mali uliofanikisha jitihada za mapambano ya ukombozi yaliyoleta uhuru kwa nchi za Kusini mwa Afrika.
Aidha, SADC imemshukuru na kumpongeza aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya Afrika, Brigedia Hashim Mbita wa Tanzania, kwa mchango wake na uongozi wake wa mapambano ya ukombozi, iwe katika nyanja ya kuviwezesha vyama vya ukombozi kwa hali na mali, raslimali na ushauri.
Pongezi hizo kwa Tanzania zilitolewa usiku wa jana, Jumamosi, Agosti 16, 2014, na Kikao cha Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC – SADC Troika- kilichofanyika kwenye Hoteli ya Elephant Hills Resort, Victoria Falls, Zimbabwe, chini ya Uenyekiti wa Rais Hifikepunye Phohaba wa Namibia.
Mkutano huo wa SADC Troika ulihudhuriwa na wanachama wa Asasi hiyo – nchi za Namibia, Lesotho na Tanzania. Nchi za Afrika Kusini, Madagascar na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilishiriki kama waalikwa maalum wa kikao hicho.
Akizungumza kwenye mkutano huo kwa niaba ya nwenzake, Rais Pohamba alisema: "Tunawashukuru wananchi wa Tanzania kwa mchango wao wa kiuchumi, kijeshi na kimkakati katika kuunga mkono kwa hali na mali jitihada za mapambano ya ukombozi wa nchi zetu."
Aliongeza Rais Pohamba: "Sote tunaijua Tanzania, sote tunawajua Watanzania.  Kwa pamoja walitoa jasho na damu na sisi wenyewe katika kutafuta ukombozi wa nchi zetu. Tutaendelea kukumbuka na kuenzi mchango wao mkubwa na usiosahaulika kwa ustawi wa nchi zetu."
Kuhusu Mzee Mbita, ambaye Ripoti yake ya shughuli za ukombozi ilitarajiwa kuwasilishwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa SADC, Rais Pohamba alisema: "Brigedia Mbita alifanya kazi mchana na usiku kufanikisha shughuli za ukombozi wa Kusini mwa Afrika. Tunamshukuru sana kwa uongozi wake na mchango wake mkubwa katika kuleta uhuru wa nchi zetu."
Aliongeza: "Brigedia Mbita ni raia wa Tanzania na alikuwa Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi Kusini mwa Afrika iliyokuwa na makao makuu yake mjini Dar es Salaam. Alichapa kazi kweli kweli na chini ya uongozi wake, vyama vya ukombozi vilipata misaada ya hali na mali, misaada ya kiroho na ushauri wa kijeshi kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa mtu wa shughuli za jeshi." Mzee Mbita aliongoza Kamati ya Ukombozi tokea mwaka 1974 hadi ilipomaliza shughuli zake.
Akizungumza kwa ufupi sana katika kikao hicho, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alimpongeza sana Brigedia Mbita akisema kuwa alifanya kazi nzuri na kubwa na "tunampogeza kwa kazi nzuri sana ya kuandaa Ripoti hiyo."
Ripoti hiyo inayojulikana kama Mradi wa Hashim Mbita iliongozwa na Meneja wa Mradi, Profesa Arnold Temu wa Tanzania na imechapishwa na Kampuni ya Mkuki na Nyota, pia ya Tanzania, ambayo Mtendaji Mkuu wake, Mzee Walter Bgoya ameandamana na mwakilishi wa Mzee Mbita kwenye mkutano huo.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.

17 Agosti,2014
Posted: 17 Aug 2014 11:03 AM PDT
 
 Baadhi ya Wasanii waliokuwa kwenye onesho la Kilimanjaro Music Tour lililofanyika mkoani Dodoma jana,leo walipitia nyumbani kwa Mfalme wa Rhymes a.k.a Simba Mzee a.k.a Afande Sele kumpa mkono wa pole na kumfariji kufuatia kifo cha Mzazi mwenzake Mama Tunda kilichotokea mwisho mwa wiki mjini Morogoro.Pichani ni Msanii wa Muziki wa Bongofleva atambulikae kwa jina la Shilole akimfariji Afande Sele
 Malkia wa Taarab hapa nchini,Bi Khadija Kopa akimfariji Afande Sele,pichani nyuma ya Afande Sele ni guli wa muziki wa Reggae hapa nchini ,Innocent Nganyagwa.
 Afande Sele akifarijiwa na mkali wa hip hop katika anga ya muziki wa Bongofleva,Joh Makini
  Baadhi ya Wasanii waliokuwa kwenye onesho la Kilimanjaro Music Tour lililofanyika mkoani Dodoma jana,wakiwa katika picha ya pamoja na Afande Sele mara baada kupitia nyumbani kwa msanii huyo na kumpa mkono wa pole na kumfariji kufuatia kifo cha Mzazi mwenzake Mama Tunda kilichotokea mwisho mwa wiki mjini Morogoro.
 Pichani ni mmoja Wanahabari kutoka gazeti la Mwananchi na Efm,Henry Mdimu,Joh Makini pamoja na Ben Paul wakiwa katika picha ya pamoja.
Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumfariji Afande Sele.Picha zote kwa hisani ya Dj Choka aliyekuwepo kwenye msafara huo,Afande Sele aliwashukuru Marafiki,washabiki wake ndugu jamaa na Marafiki kwa umoja na mshikamano waliouonesha kwake katika kipindi hiki kigumu ambacho hakikuwahi kumtokea katika maisha yake ya kuondokewa na Mpendwa Mke/mzazi mwenzake. '' sina maneno yanayoweza kuelezea kwa wepesi faraja,upendo na ushirikiano nilioupata kutoka kwenu,nawashukuruni sana ndugu zangu'' ,alimaliza kusema Afande Sele huku akionekana kuwa mwenye simanzi kubwa
Posted: 16 Aug 2014 09:12 PM PDT
Posted: 17 Aug 2014 09:47 AM PDT
Bodi ya korosho Nchini Imetangaza Kuanza rasmi kwa ununuzi na uuzaji wa korosho katika msimu wa 2014/2015 utakaonza tarehe 20 mwezi huu ili wakulima waweze kuitumia vema fursa ya kuvuna mapema korosho zao kabla ya nchi nyingine kuanza kuvuna. 
Mwenyekiti wa bodi ya korosho Tanzania Mhe Anna Abdallah (MB)ameyasema hayo akiongea na waandishi wa habari na kubainisha kuwa ili kufikia azima hiyo ya kutumia fusa ya uvunaji mapema ni vizuri wadau wote wanaohusika na uuzaji na ununuzi wakamilishe maandalizi muhimu kabla ya msimu kufunguliwa rasmi ili kuepuka ucheleweshaji wa ununuzi na uuzaji wa korosho msimu huu.
 Kufuatia kikao cha wadau wa tasnia ya zao la korosho katika mkutano wao mkuu wa mwaka uliofanyika mjini Masasi tarehe 9-10 mwezi huu wakulima walikubaliana kuwa bei dira(mwongozo)ya korosho ghafi daraja la kwanza kuuzwa na kuanzia tshs shilingi 1000/= kwa kila kilomoja.
Ambapo korosho daraja la pili zitauzwa na kununuliwa kwa shilingi 800/= kwa kila kilo moja ambapo alifafanua kuwa kuwa bei hizo ni za mwongozo tu kwani bei halisi itategemea nguvu ya soko ambapo inaweza kubadilika kutokana na Ushindani wa wanunuzi kupitia minada 
Aidha mwenyekiti huyo aliwataka wafanya biashara kujiandaa kufanya malipo ya leseni za biashara hiyo kufuatia miaka ya nyuma leseni za biashara zilikuwa zinatolewa bila malipo.
Hata hivyo kwa mujibu wa sheria ya fedha namba 5 ya mwaka 2011,kuanzia msimu huu leseni za ununuzi wa zao hilo zitatolewa kwa malipo Ambapo wanunuzi wa ndani watalipia ada ya shilingi 750,000/= na wanunuzi wa nje walipia ada ya dola za kimarekani 500/= kwa msimu Ununuzi wa zao hilo umekuwa ukiyumba katika baadhi ya misimu hasa kuhusiana na suala la bei kiasi cha kusababisha malalamiko na migogoro hata vurugu kutoka kwa wakulima dhidi ya serikali,vyama vya msingi na Ushirika 
Awali katika mkutano wa wadau wa korosho, BODI zote za mazao nchini zimetakiwa kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wakulima ili kuwajengea matumaini ya kuzalisha kwa wingi na kwa viwango vinavyohijtajika kwenye masoko ya ndani na nje na kuliletea taifa fedha za kigeni. Rai hiyo ilitolewa wilayani Masasi mkoani Mtwara na waziri wa kilimo,chakula na Injinia Christopher Chiza alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa wadau wa korosho Tanzania uliofanyika wilayani Masasi katika ukumbi wa Emirates  
Waziri Chiza Alisema kuwa bodi zote za mazao hapa nchini zinatakiwa zitatuwe matatizo ambayo wakulima wanakumbana nayo na kuwasababishia washindwe kufikia malengo yao waliyoyakusudia kunakotokana na viongozi wa bodi kukwepa kutimiza majukumu yao wanayotakiwa kuyatekeleza. "Kwa sasa kumekuwa na mwaya mkubwa kati ya bodi, Halmashauri za wilaya na miji,mifuko ya pembejeo na wakulima inayosababishia kutofanya vizuri na kumuacha mkulima akiwa kisiwani bila ya kupata msaada kupitia bodi hizo hivyo suala kubwa ambalo linapelekea kuwepo na mwanya huyo kunatokana na kutowashirikisha wakulima kwenye maamuzi mbalimbali ikiwemo kwenye kufanya mahesabu ya uendeshaji yanayohusu manunuzi,gharama za matumizi na malipo ya majaliwa ambayo ni kiini cha mafanikio kwa mkulima wa mazao.
"Wakulima wa Tanzania wako tayari kuzalisha bidhaa za mazao yao na Ili mkulima apewe matumaini ya kuzalisha mazao kwa tija bodi lazima ziwe mstari wa mbele katika utendaji wa majukumu yake kwa ufanisi na uaminifu zaidi na kutii sheria ya ushirika na kanuni zake kwakufanya hivi kutamsaidia mkulima,"alimalizia Waziri Chiza
Mwenyekiti wa bodi ya korosho Mhe Anna Abdallah  akifungua kikao cha wadau wa korosho kilichofanyika wilayani Masasi mkoani Mtwara kulia ni waziri wa kilimo na ushirika Injinia Christopher Chiza na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Joseph Simbakalia. Kikao hicho kinajadili maendeleo na changamoto za zao hilo
Posted: 17 Aug 2014 09:38 AM PDT
UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union "Wagosi Kaya" umekanusha vikali taarifa zilizizoenezwa kuwa mlinda mlando wa kikosi cha Vijana wenye umri chini ya miaka ishirikini U-20 Fikirini Suleimani "Mapara" kuwa amesajiliwa na Klabu ya African Sports "Wanakimanumanu"

Umesema taarifa hizo hazina ukweli wowote bali Fikirini bado ni mchezaji halali wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga na ni miongoni mwa wachezaji watakaoonekana kwenye kikosi hicho msimu ujao.

Taarifa iliyotolewa leo kwa nyombo vya Habari kupitia msemaji wa Klabu hiyo Oscar Assenga zimeelezwa kuwa fikirini bado ni mchezaji halali wa timu hiyo kwa kusajiliwa hivyo taarifa ya kuwa amejiunga na Africa Sports hazina ukweli wowote ule.

 Assenga amesema kuwa ili wadau wa soka waweze kuthibitisha kuwa mchezaji huyo bado yupo kwenye kikosi cha wagosi hao wa kaya wafike mazoezini Jumatatu kwani atakuwepo.

Amesema kuwa Fikirini ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo msimu ujao wa Ligi kuu soka Tanzania bara.
Posted: 17 Aug 2014 09:27 AM PDT
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO 
Serikali itaendelea kutoa mafunzo kwa watendaji wa Halmashauri na Mikoa juu ya usimamizi wa fedha, manunuzi na takwimu katika masuala ya elimu nchini ili kuwajengea uwezo viongozi hao katika masuala ya usimamizi wa fedha za Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari awamu ya pili (MMES II). 
 Kauli hiyo imetolewa mjini Bagamoyo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia wakati akifunga mafunzo ya viongozi wa elimu ngazi ya mikoa. 
 Ameongeza kuwa mafunzo hayo yanalenga kuboresha ujuzi na utendaji kazi wao ili kukabiliana na changamoto zilizopo. 
 Waziri Ghasia amewasihi watendaji hao kuwa washirikiane katika kutekeleza majukumu yao, kwani lengo ni kufanya kazi kwa pamoja ambapo kila mtu anafahamu majukumu yake na mipaka yake ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. 
 Katika hatua nyingine Waziri Ghasia amesema kuwa kulingana na Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, jumla ya watu milioni 14,796,537 ambao ni sawa na asilimia 34 wa kuanzia  shule za awali, msingi na sekondari zinazosimamiwa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa. 
Amefafanua idadi hiyo kuwa watu wa umri wa miaka 5 hadi 6 idadi yao ni 2,755,699 ambao ni sawa na asilimia 6.32, miaka 7 hadi 13 idadi yao ni 8,341,701 ambao ni sawa na asilimia 19.12, miaka 14 hadi 17 idadi yao ni 3,699,137 ambao ni sawa na asilimia 8.48. 
Mhe  Ghasia ameongeza kuwa taarifa hizo ni muhimu katika kuiwezesha Serikali kupanga mipango yote ya kuwaendeleza watu hao katika nyanja zote. 
 Mafunzo hayo yaliwashirikisha Maafisa Elimu na Afisa Mipango wa mkoa 16 pamoja na Maafisa Elimu wilaya, Wahandisi, Waweka hazina pamoja na Maafisa Elimu Vifaa na Takwimu kutoka halmashauri za mikoa hiyo. 
Baadhi ya mikoa ambayo watendaji wake walishiriki mafunzo hayo ni Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Singida, Kigoma, Manyara, Arusha, Mbeya, Kilimanjaro, Kigoma, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Geita.
 1.      Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia akiwaasa washiriki wa mafunzo katika masuala ya usimamizi wa fedha za MMES II kutoka mikoa 16 nchini ambao ndio watendaji wakuu katika usimamizi wa elimu, wamo Maafisa Elimu na Afisa Mipango mkoa pamoja na Maafisa Elimu wilaya, Wahandisi na Waweka hazina kutoka halmashauri za mikoa hiyo. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi.
 Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa elimu ngazi ya mikoa katika masuala ya usimamizi wa fedha za MMES II wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia wakati wa kufunga mafunzo hayo hivi karibuni katika chuo cha Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Bagamoyo.
1.      Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia akiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa mafunzo usimamizi wa fedha za MMES II kutoka  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, TAMISEMI na chuo cha ADEM pamoja na baadhi ya wanasemina hivi karibuni Bagamoyo.
Posted: 17 Aug 2014 08:44 AM PDT
 Immaculate Makilika –MAELEZO_DAR ES SALAAM 
WAZEE wa Mkoa wa Dar es salaam wamewaomba Umoja wa Katiba wa Wananchi (UKAWA) kurudi Bungeni ili kuendelea na mchakato wa majadiliano ya Rasimu ya Katiba Mpya yanayoendelea. 
 Wazee hao wamesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya siasa nchini pamoja na Bunge la Katiba Mpya linaloendelea mjini Dodoma. Akizungumza kwa niaba ya Wazee wenzake Kepteni Mstaafu Alhaji Mohamedi Ligora , amesema kuwa Tanzania ni nchi nzuri na watu wake ni wazuri ni vema UKAWA na wenzao wakarudi Bungeni kujadiliana ili watimize matakwa ya kidemokrasia. 
 Amesema kuwa wananchi wa Tanzania hawataki kufananishwa na nchi zingine zilizofanya makosa na kupata matatizo kutokana na mambo kama haya ambayo yalisababisha wananchi wao kuzikimbia nchi zao kwa mambo ambayo wangeweza kukaa chini na kumaliza wenyewe kwa ajili ya maslahi ya umma. Kapteni Mstaafu Alhaji Ligora amesema kuwa suala la mchakato ni suala la kidemokrasia, hivyo ni vyema UKAWA wakatumia fursa hiyo waliyonayo kwa kurudi Bungeni na kuendelea na majadiliano kuhusu Rasimu ya Katiba hali itakayosaidia kupatikana kwa Katiba Mpya ambayo itakuwa na manufaa kwa wananchi wa Tanzania. 
 Aidha, amewaomba wajumbe walio Bungeni na wale walio nje ya Bunge kuacha kuwazomea UKAWA badala yake wawasihi warudi katika chombo rasmi cha kuboresha Rasimu ya Katiba Mpya. 
 Naye Mzee Ali Bakari Muki, amewataka UKAWA kuheshimu misingi ya demokrasia lakini pia amewapongeza wabunge walioitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kurudi Bungeni na kuendelea na majadiliano kuhusu Katiba kwani ndio Jukwaa pekee la kuwapatia wananchi Katiba bora. 
 Kwa upande wake Mzee Yahaya Ngoma amewataka viongozi wote hasa UKAWA kuheshimu na kudumisha jitihada zilizofanywa na waasisi wa Taifa hili akiwemo Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere pamoja na Sheikh Abeid Amani Karume kwa kuzingatia misingi na kanuni za uongozi bora kwa kutumia njia ya majadiliano pale panapokuwa na mawazo tofauti baina yao. Halikadhalika, Alhaji Sheikh Bakari Chikawa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuridhia kuanza kwa mchakato wa Katiba Mpya na kusisitiza ni moja ya tunda la uongozi bora na demokrasia nchini. 
 Aidha, ameongeza kuwa UKAWA ni vema wakatumia fursa hiyo ya demokrasia kwa kuwawakilisha vema wananchi wa Tanzania ili kuhakikisha wanapata Katiba Bora. Alhaji Chikawa amewaomba UKAWA kurudi Bungeni kwani kunyume na hivyo ni watakua wametenda dhambi na madhara yake ni makubwa sana, na kusisitiza kuwa mazungumzo ni muhimu na yakipuuzwa basi kuna madhara.
 Kepteni Mstaafu Alhaji Mohamed Ligora , akizungumza kwa niaba ya  Wazee wenzake  wa mkoa wa Dar es salaam walipoongea na waandishi wa habari leo ambapo amesema kuwa Tanzania ni nchi nzuri na watu wake ni wazuri ni vema  UKAWA na wenzao  wakarudi Bungeni kujadiliana ili watimize matakwa ya kidemokrasia.
  Mzee Alhaji Sheikh Bakari Chiwaka (kulia) akisisitiza umuhimu wa maridhiano katika mchakato wa Katiba Mpya na kuwa Katiba bora itapatikana kwa uongozi bora na wa kidemokrasia nchini. Kushoto ni Kepteni Mstaafu Alhaji Mohamed Ligora.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene akiwasikiliza
Wazee wa mkoa wa Dar es salaam mara baada ya mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam. Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Posted: 17 Aug 2014 08:37 AM PDT

BEAUTY AND MUSIC NIGHT. Siku zinazidi kukaribia hadi Tarehe 30 August ambapo Kwenye Stage watakuwepo Sauti Sol, Yamoto, Skylight Band pamoja na Mirror. Hii show siyo ya kukosa. Pia Kutawepo na Red Carpet na ofa ya kupiga picha kali kwa watu wote watakongia. Njoo usikilize ladha ya muziki wa live katika Stage, Sound lights za Kisasa kabisa kutoka Legendary Music Company.  
VENUE. ESCAPE 1 MIKOCHENI. 
KIINGILIO. 15,000Tshs/- 
Ticket za VIP zinapatikana kwa 50,000Tshs/- 
Unaweza kupiga simu zilizopo katika poster kwa maelezo zaidi.
Posted: 17 Aug 2014 08:34 AM PDT
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuwahudumia Wananchi wake katika kuwapatia huduma muhimu na za msingi za Kijamii ikielewa fika kwamba inatekeleza Sera na ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo hapo katika Kijiji cha Mvuleni Kidoti Wilaya ya Kaskazini "A " wakati akikabidhi vifaa mbali mbali vya ujenzi kwa ajili ya kuufanyia matengenezo makubwa Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Kijiji hicho. 
Balozi Seif alikabidhi vifaa hivyo ambavyo ni pamoja na Mabati,Miti na Papi za kuezekea, mbao,matofali, mawe, mchanga pamoja na saruji ikiwa ni awamu ya kwanza ya matengenezo hayo akianza kutekeleza ahadi aliyoitoa Tarehe 20 mwezi uliopita alipofanya ziara fupi kukagua maendeleo na changamoto zinazowakabili wananchi wa Kijiji hicho. 
Balozi Seif alisema Serikali inaelewa dhiki na matatizo ya Kiuchumi na Kijamii yanayowapata wananchi katika maeneo mbali mbali nchini. Hivyo katika kukabiliana na matatizo hayo Serikali itaendelea kuhudumia kadri hali itakavyoruhusu. 
Msimamizi wa matengenezo ya Msikiti huo wa Ijumaa wa Kijiji cha Mvuleni Bwana Khamis Yussuf Kombo kwa niaba ya waumini na wananchi wa kijiji hicho alimpongeza Balozi Seif kwa msimamo wake anaouchukuwa wa kusimamia harakati za kijamii hapa Nchini. 
Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alipata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi wa tangi kubwa la kuhifadhia maji safi na salama liliopo katika Kijiji cha Mwanguo Bwereo litakalokuwa na uwezo wa kusambaza huduma ya maji katika Vijiji mbali mbali vilivyomo ndani ya Wilaya hiyo.
 Afisa wa Maji Wilaya ya Kaskazini "A" Ndugu Dude Kidongo Amour aliyepo kati kati akitoa maelezo Mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kuhusu ujenzi wa Tangi kubwa la kuhifadhia maji linalojengwa na Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } liliopo katika Kijiji cha Mwanguo Bwereo.
 Balozi Seif akikamilisha kukagua tangi la kuhifadhia maji safi na salama la Mwanguo Bwereo litakalohudumia huduma hiyo kwa wananachi wa Vijiji mbali mbali vilivyomo ndani ya Wilaya ya Kaskazini "A ".
 Balozi Seif akibadilishana mawazo na Imamu Mkuu wa Msikiti wa Ijumaa wa Kijiji cha Mvuleni SheikhKhamis Duchi Kheir kabla ya kukabidhi vifaa mbali mbali kwa ajili ya matengenezo makubwa ya msikiti huo.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimkabidhi Imamu wa Msikiti wa Ijumaa wa Mvuleni Sheikh Khamis Duchi Kheir vifaa mbali mbali vya ujenzi wa msikiti huo.
 Balozi Seif akiambatana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Nd. Haji Juma Haji wakielekeakuzungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mvuleni mara baada ya kukabidhi vifaa vya ujenzi wa msikiti wa Kijiji hicho.
 Balozi Seif akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mvuleni Kidoti mara baada ya kuanza kutekeleza ahadi yake aliyoitoa ya kusaidia matengenezo makubwa ya Msikiti wa Ijumaa wa Kijiji hicho. Kushoto ya Balozi ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Nd. Haji Juma Haji na Afisa Tawala wa Mkoa huo Dr. Makame Shauri. Picha na Hassan Issa wa OMPR, ZNZ.      
Posted: 17 Aug 2014 08:08 AM PDT

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeamua kurejesha ofisi zake Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume kwa vile mipango ya uendelezaji wa eneo hilo bado haijakwenda kama ilivyopangwa awali.
 Uamuzi huo ni moja ya maazimio yaliyofikiwa kati ya Kamati ya Utendaji ya TFF na ujumbe wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) uliokuwepo nchini kwa wiki nzima kwa ajili ya kufanya mapitio (review) ya uendeshaji wa TFF. 
Akizungumza Dar es Salaam leo (Agosti 17 mwaka huu), kiongozi wa ujumbe huo wa FIFA uliokuwa na maofisa sita, Zelkifli Ngoufonja amesema wamepitia maeneo mbalimbali ya uendeshaji wa TFF na mpira wa miguu kwa ujumla na kukubaliana kufanya uboreshaji kwa lengo la kuongeza ufanisi. 
Ngoufonja ambaye ni Meneja Mwandamizi wa FIFA anayeshughulikia Programu za Maendeleo Afrika amesema kabla walikutana na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali kwa lengo la kuangalia jinsi watakavyochangia katika uendelezaji mpira wa miguu nchini. 
Amesema wamekubaliana na TFF katika mpango wa utekelezaji (Action Plan) na maazimio waliyokubaliana ikiwemo na muda wa utekelezaji wake, hivyo FIFA watafuatilia na kutoa msaada ili kuhakikisha utekelezaji unafanyika kama ilivyopangwa. 
Maeneo yaliyofanyiwa kazi ni utawala bora (Governance), Maendeleo ya Ufundi (Technical Development), timu za Taifa (National teams), Mashindano na Vitendea Kazi (Competitions and Facilities), na Utawala na Uongozi (Administration and Management). 
Maofisa wengine wa FIFA waliofuatana na Ngoufonja ambaye ni raia wa Cameroon ni Meneja wa Programu za Ustawi (Performance), Marco Schuepp, Ofisa Maendeleo, Ashford Mamelodi, Ofisa Maendeleo wa Ufundi, Govinden Thondoo, Mkufunzi wa Makocha, John Peacock na Mshauri wa Programu za Ustawi, Ian Riley.

MUDA WA USAJILI WAONGEZWA KWA SIKU KUMI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeongeza kwa siku kumi muda wa kumalizika usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL)  kutokana na kuchelewa kwa link ya mfumo mpya wa usajili (system) kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF). 
Kwa mujibu wa CAF, link hiyo itakuwa tayari kwa matumizi ndani ya siku tatu zijazo kutokana sasa. Hivyo, mameneja wa usajili wa timu hizo kwa sasa wanatakiwa kukamilisha nyaraka zote zinazotakiwa ili link hiyo itakapokuwa tayari waweze kuingiza usajili wao mara moja. 
Kuanzia msimu wa 2014/2015 mfumo unaotumika kwa usajili kwa klabu hizo ni wa elektroniki badala ya ule wa zamani wa kutumia fomu za kawaida. Mfumo huo wa kisasa ambao pia unatumiwa na CAF unaondoa upungufu uliokuwepo katika mfumo wa zamani. 
Kutokana na mabadiliko hayo, usajili sasa utamalizika Agosti 27 mwaka huu badala ya leo (Agosti 17 mwaka huu). Kipindi cha pingamizi ni kuanzia Agosti 28 mwaka huu hadi Septemba 3 mwaka huu.
 Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itakutana kati ya Septemba 6 na 8 mwaka huu kwa ajili ya kupitia pingamizi na kuthibitisha usajili.
 Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoshirikisha timu 14 itaanza Septemba 20 mwaka huu wakati ratiba inatarajia kutoka mwezi mmoja kabla ya kuanza ligi hiyo. Ligi Daraja la Kwanza inatarajia kuanza wiki ya kwanza ya Oktoba. 
Mwisho wa kuombewa Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) kwa wachezaji wanatoka nje ya Tanzania ni Septemba 6 mwaka huu.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


Posted: 17 Aug 2014 07:01 AM PDT
Naibu waziri maji Amos Makalla leo ameongoza waumini wa kanisa kkkt dayosisi ya mashariki , viongozi wa majimbo na sharika zake katika harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa shule ya Elbeneza itakayokuwa kwa ajili ya shule ya msingi na sekondari. 

Katika harambee hiyo fedha sh 124m zilipatikana kati ya hizo fedha taslimu sh 57m zilipatikana na 67m ikiwa ni ahadi. lengo la harambee ni kupata sh 120m kukamilisha majengo muhimu kuwezesha shule hiyo kufunguliwa januari mwakani. 

Makalla alimpongeza askofu mameo, wachungaji na waumini kwa michango yao kufanikisha ujenzi Aidha alilipongeza kanisa kwa uumuzi wa kujenga shule imeonyesha namba kanisa lilivyo tayari kushirikiana na serikali na amewahaidi kuzitafutia changamoto mbalimbali walizompatia kuziwasilisha serikalini.
Naibu Waziri Maji,Mh. Amos Makalla akitoa neno kwa ajili ya harambee ya kanisa la kkkt Bungo -Morogoro.
Naibu Waziri Maji,Mh. Amos Makalla akishiriki ibada ya harambee kanisa la kkkt Bungo-morogoro.
Naibu Waziri Maji,Mh. Amos Makalla akipata mkono wa baraka kutoka kwa baba askofu wa dayosisi ya mashariki baada ya harambee kanisa la Bungo- morogoro.
Posted: 17 Aug 2014 06:54 AM PDT
Mkuu wa wilaya Ya Kilwa ,Abdallah Ulega (kushoto) akipokea sehemu ya mchango uliotolewa na Kampuni ya uchimbaji gesi ya PANAFRICAN ENERGY kutoka kwa Meneja wa huduma za jamii wa kampuni hiyo,Andrew Kashangaki .

Na Abdulaziz Kilwa Masoko

Wananchi wilayani Kilwa mkoani Lindi wameendelea kunufaika na wawekezaji,baada ya kampuni ya uchimbaji gesi ya PANAFRICAN ENERGY kuikabidhi halmashauri hiyo zahanati ya kijiji cha Nangurukuru ambayo ujenzi wake umegharimu Tshs 262 Milioni .

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo ambayo yalifuatiwa na utiaji sahihi mkataba wa ujenzi wa nyumba mbili za watumishi wa zahanati hiyo ambazo ujenzi wake hadi kukamilika utagharimu shilingi 458 milioni Meneja wa huduma za jamii wa kampuni hiyo,Andrew Kashangaki alisema katika ujenzi wa zahanati hiyo kampuni ya PANAFRICA N imechangia jumla ya shilingi 216,000,000.

Ambapo pia kutokana na tatizo la wafanyakazi pia kampuni imeamua kufadhili ujenzi wa nyumba mbili za watumishi wa zahanati hiyo ambazo mkataba wenye thamani ya shilingi 458,000,000 ulisainiwa baina ya mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bw David Roberts na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa katika hafla hiyo fupi ya kukabidhi zahanati.

Aidha Kashangaki alibainisha kuwa sera ya kampuni hiyo licha ya kufanya kazi ya uzalishaji wa Gesi ya songosongo pia hutoa misaada kwa jamiii ikiwemo kufadhili programu ya ufundishaji lugha ya kiingereza kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza wa shule za sekondari za halmashauri hiyo,ambapo jumla ya shule za sekondari 20 kati ya 28 zimenufaika na programu hiyo.

'Wana kilwa tulianza kusaidia elimu ya kiingereza kwa kuzifikia shule 20 ila kwa umuhimu wa elimu kuanzia mwakani tutazifikia shule zote 28 za sekondari ikiwemo kusaidia upatikanaji wa Umeme Jua kwa shule ambazo hazina umeme 'Alimalizia Kashangaki.

Mkuu wa wilaya Ya Kilwa ,Abdallah Ulega licha ya kuishukuru kampuni hiyo aliwataka wananchi kupuuza kauli zinazosemwa ikiwemo baadhi ya Vyombo vya habari kupotosha na kudai Manufaa ya Gesi yapo katika kijiji cha Songosongo pekee Na kubainisha baadhi ya maeneo yanayonufaika ikiwemo hapo Nangurukuru,Njinjo ,Somanga na kilwa masoko

'Wananchi wa Kilwa nadhani ni mashahidi kampuni hii imesaidia wilaya yote si Kama Gazeti moja lilivyoandika hivi karibuni Huu ni upotoshaji mkubwa kwani elimu inasaidiwa wilaya yote,Afya Hivyo hivyo,Maji wananufaika mpaka Njinjo na hata mrahaba unaolipwa na kampuni hiyo zaidi ya Nusu inachangia katika sekta ya elimu Tuwe makini kuyajua haya yenye ukweli si maneno tu ya vijiweni...Alimalizia Ulega.

Awali akifungua hafla hiyo Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Nangukuru,Hamis Ligweje alisema kabla ya PANAFRICAN kufadhili ujenzi huo,wananchi wa kijiji hicho kwa kushirikiana na wahisani wengine ikiwamo shirika la Action Aid walichangia walichangia jumla ya shilingi Milion 46 ujenzi ambao ulikuwa wa kusuasua mpaka wahisani hao walipojitokeza kusaidia kuikamilisha.

'Hakika tulishindwa kabisa na Tulifikia hatua ya Kumuomba Rais Kikwete Kusaidia alipokuja katika ziara yake ambapo aliwaagiza Viongozi wa Wilaya kuangalia uwezekano ndipo Mkurugenzi aliehama Bw Mapunda Alifanikisha kuwaomba hawa wahisani na leo wametukamilishia na tunafarijika zaidi walipoamua kutujengea na Nyumba 2 kwa 4 za watumishi itasaidia sana si kwa Nangurukuru tu hata wasafiri watakaopata dharula katika barabara kuu.

Licha ya kukabidhi Zahanati hiyo Mkurugenzi mkuu wa Pan African Energy,David Roberts Alikabidhi Vitanda Viwili vya kujifungulia akina mama ikiwa ni hatua ya awali ya kuokoa Akina mama katika suala la Uzazi.
Posted: 17 Aug 2014 05:45 AM PDT


Na Mwandishi Wetu
BODI ya Wadhamini ya Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB), imemteua  Jaji wa Mahakama ya Rufaa nchini, Dk.Stephen Bwana Kuwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la chuo hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB), Mikocheni Dar Es Salaam, Dk.William Kudoja alisema  Bodi ya Wadhamini ya chuo hicho ambayo Inaongozwa na Professa Paramaganda Kabudi Ndiyo ilimteua Jaji Bwana kushika wadhifa huo mpya baada ya kuona Ana sifa za vigezo Vya kushika wadhifa huo.

Dk.Kudoja ambaye ni Naibu Makamu Mkuu wa UB anayeshughulikia Taaluma, alisema jaji Bwana ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa  ya Jinai (ICC) ya nchini Cambodia.

Jaji Bwana aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali Kama Jaji wa Mahakama Kuu  Seychelles 1994-1999, Jaji wa Mahakama Rufaa ya Seychelles 2004-2009 , Kaimu wa Rais wa Mahakama hiyo ya Rufaa ya Seychelles kuanzia  Mwaka 2006-2008.

Mbali na kushika nyadhifa hizo Jaji Dk.Bwana  pia aliwai Kuwa Mshauri wa Benki ya Dunia kuhusu  Uboreshaji  wa Shughuli za Mahakama Afrika Kati ya Mwaka 2003-2008, Msajili wa Mahakama ya rufaa nchini Mwaka 1989-1994 na Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania  Mwaka 1989  na Hakimu na Hakimu Mkazi Mwaka 1974.

Dk.Kudoja alisema Mwenyekiti huyo wa Baraza la UB, Jaji Bwana atawaongoza wajumbe  wajumbe 19 wa Baraza Hilo kutekeleza majukumu hayo ambao nao wanapitishwa na Bodi ya Wadhamini wa chuo hicho na watatekeleza majukumu waliyopewa.

Mbali na Jaji Bwana  Alisema wajumbe wa Baraza Hilo ni Profesa Esther Mwaikambo kutoka Taasisi ya Vyuo Vikuu Binafsi(IES), Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya juu nchini, Dk.Sylvia Temu, Mkurugenzi Mtendaji Mstaafu wa Kituo Cha Uwekezaji nchini(TIC), Emmanuel Ole Naiko, Vicent Jonas, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi, George Simbeye, Wakili Mwandamizi wa Serikali Malata Gabriel , Mhadhiri wa Sheria wa chuo hicho, Baraka Mkami, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Halima Kihemba, Makamu Mkuu wa chuo hicho ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge la Katiba, Profesa Costa Mahalu, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mercy Sila, Dk.William Kudoja.

Aidha Alisema wajumbe wengine ni Naibu Makamu Mkuu wa UB anayeshughulikia Fedha, Dk. Elifuraha Mtalo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu  Cha Kilimo Sokoine  anayeshughulikia Taaluma Profesa Peter Gillah, Mwenyekiti wa Kampuni ya Proin Promotions Limited Johnson Lukaza, Mathias Massawe, Mkurugenzi wa Sayansi na Teknolojia Katika Wizara ya  ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Evelyn Mbede, Balozi na Wakili mwandamizi nchini Mwainaidi Sinare Maajar, Wakili wa kujitegemea Vulfrieda Mahalu na Mkuu wa Shule ya Elimu ya UB, Profesa Elias Bayona.
Posted: 17 Aug 2014 05:42 AM PDT
Paulina Nyoni (Mama wa mtoto Fatuma Msuya) akiwa amembeba mwanaye ambaye anahitaji msaada wa matimabu .
----------------------
Paulina nyoni mkazi wa kijiji cha Hanga wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma anaomba msaada kwa yeyote atakaye guswa na tatizo la mwanaye  aitwaye Fatuma Msuya ili aweze kupata matibabu katika hospitali ya KCMC moshi.

Paulina ni mama mwenye watoto wa tano anayejishugulisha na kilimo , Mume wake aitwaye  Jafari Msuya amemtelekeza baada ya kujifungua mtoto mwenye tatizo hili na kukimbia kusikojulikana hivyo kumfanya mama wa mtoto huyu kutokuwa na msaada wowote ule,

Fatuma Msuya (1) amezaliwa tarehe 24/2/2013 katika Hosptali ya mkoa wa Ruvuma akiwa na tatizo la kutokuwa na sehemu ya kutolea haja kubwa na hivyo kulazimika kufanyiwa upasuaji tumboni ambapo kwa sasa anatolea haja kubwa,awali kabla ya kupasuliwa alikuwa akitolea haja kubwa sehemu ya aja ndogo.

Upasuaji wa awali alifanyiwa katika Hospitali ya Mission Peramiho iliyopo wilaya ya songea tarehe 19 04/ 2013
Na kwa sasa mtoto huyu anakabiliwa na tatizo jingine la kutokwa na vidonda sehemu anayojisaidia  hali inayomsababishia maumivu wakati wote na anapojisaidia haja kubwa hutokwa na damu.

Gharama za matibabu zinazohitajika  ni shilingi milioni tatu, Yeyote atakayeguswa anaweza kutoa msaada kwa Mpesa no 0767 710 113 .
"Kutoa ni moyo"
Posted: 17 Aug 2014 05:34 AM PDT
Waziri Mkuu, Mizewngo Pinda (wa tatu kulia) akikagua ujenzi wa daraja la kigamboni jijini Dar es salaam August 16, 2014.
Waziri Mkuu, Mizewngo Pinda akisalimiana na baadhi ya wataalam wa ujenzi wa nyumba hizo unaofanywa na Shirika la NSSF katika eneo la Kigamboni jijini Dar es salaam August 16, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua ujenzi wa nyumba unaofanywa na Shirika la NSSF katika eno la Kigamboni jijini Dar es salaam August 16, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na Bibi Doreene Mkandara na Mwanae Adastus Aporinary ambao ni miongoni mwa wateja waliouziwa nyumba na Shirika la Nyumba la Taifa la NHC zilizoko eneo la Kibada Kigamboni jijini Dar es salaam ambako Waziri Mkuu aliembelea August 16, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Meck Sadik na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema (kushoto) kukagua nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa NHC zilijengwa na kuuzwa eneo la Kibada Kigamboni jijini Dar es salaam August 16, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua ujenzi wa nyumba katika mradi wa DEGE ECO VILLAAGE unaomilikiwa na Shirika la NSSF eneo la Kigambaoni August 16, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Posted: 17 Aug 2014 05:33 AM PDT
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisisitiza jambo baada ya kupata maelezo juu ya maendeleo ya Mradi wa Daraja la Kigamboni kabla ya kufanya ziara ya siku moja ya kutembelea Miradi iliyofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar es Salaam. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadani Dau (kushoto) akitoa maelezo juu ya miradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village modern city Housing scheme' yenye thamani ya matrilioni. Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikuwa na ziara ya siku moja ya kutembelea miradi mikubwa ya miundombinu ya mfuko huo jijini Dar es Salaam.
 Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni Mhandisi Karim Mattaka (kulia) akimuonyesha Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wapili kulia) mchoro sanifu wa daraja la Kigamboni, wakati wa ziara ya waziri mkuu kutembelea miradi mitatu mikubwa  inayofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar es Salaam.
 Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni Mhandisi Karim Mattaka (kulia) akimuonyesha Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wapili kulia) hatua za ujenzi wa daraja la Kigamboni, wakati wa ziara ya waziri mkuu kutembelea miradi mitatu mikubwa  inayofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wapili kulia) akitembelea mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni unaofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa ziara yake ya siku kutembelea miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda (Watano Kulia) katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali na wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mara baada ya kutembelea mradi wa daraja la Kigamboni ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi. 
Posted: 17 Aug 2014 05:11 AM PDT
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi alisema kwamba utitiri wa vyuo vikuu bila ya ubora wa elimu inayotolewa ni jambo linalopelekea vyuo hivyo kutoa vijana wasiouzika kiajira katika taasisi mbali mbali za umma na hata zile za binafsi.

Mama Asha Suleiman Iddi alisema hayo wakati wa hafla maalum ya kuagana kwa wana jumuiya ya wanafunzi wa Zanzibar wanaosoma chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro wa ZAMUMSA ambao wanatarajiwa kumaliza mafunzo yao mwezi Novemba mwaka huu iliyofanyika katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar uliopo Kikwajuni Mjini Zanzibar.

Katika kuunga mkono jumuiya hiyo ya wanafunzi wa Zanzibar wanaosoma chuo kikuu cha Kiislamu Mkoani Morogoro Mke huyo wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha aliahidi kuipatia mchango wa Kompyuta, Printa na Mashine ya Fotokopi Jumuiya hiyo ili ipate nguvu zaidi za kiutendaji.

Hata hivyo Mama Asha aliwaasa na kuwatahadharisha wanafunzi hao wa elimu ya juu kujiepusha na ushawishi wa wanasiasa kwa kuwatumia kujiingiza katika matendo maovu ya uvunjifu wa amani ya Nchi.

Akisoma risala ya wanajumuiya hiyo ya Wanafunzi wa Zanzibar wanaosoma Chuo Kikuu cha Kiislamu Mkoani Morogoro { ZAMUMSA } Mwanajumuiya Saleh Haji alisema lengo la kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo mwaka 2006 ni kuwaunganisha pamoja wanafunzi wote ili kuwa rahisi kukabiliana na changamoto wanazopambana nazo.

Mapema Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Zanzibar wanaosoma chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro Hamad Ali alisema wanajumiya hao wameamua kujitolea kuitumikia nchi yao licha ya changamoto wanazopambana nazo.

Hamad Ali alisema wanafunzi hao wanahitaji kuitumia taaluma waliyojifunza kwa kuisaidia jamii iliyowazunguuka katika maeneo yao.
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Zanzibar wanaosoma chuo kikuu cha Kiislamu Morogoro Nd.Kassimu N'gwali akitoa neno la shukrani kwa waalikwa wa hafla yao ya kuagana kwa wanajumiya wanaomaliza masomo yao mwezi Septemba mwaka huu wa 2014. Kulia ya Ndugu N'gwali ni Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae ndie mgeni rasmi wa hafla hiyo Mama Asha Suleiman Iddi.
Baadhi ya wana jumuiya ya wanafunzi wa Zanzibar wanaosoma chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro wakifuatilia hafla ya maagano kwa wanajumiya wanaotarajiwa kumaliza mafunzo yao mwezi Septemba mwaka huu.
Mwanajumiya ya ZAMUMSA Saleh Haji alitaja baadhi ya changa moto wanazopakabiliana nazo wakati akisoma Risala ya jumiya hiyo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Mwenyekiti wa ZAMUMSA Bibi Saada akimkabidhi zawadi Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi kwenye hafla ya kuagana wanajumiiya hiyo wanaomaliza masomo yao mwezi Septemba mwaka huu.
Mama Asha Suleiman Iddi akizungumza na Wana Jumuiya ya ZAMUMSA kwenye ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi uliopo Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Mama Asha akimkabidhi Cheti Maalum Mwenyekiti mstaafu wa ZAMUMSA Nd. Rashid Mjaka kwa niaba ya viongozi wenzake baada ya kumaliza muda wao wa utumishi wa jumuiya hiyo. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Posted: 17 Aug 2014 04:57 AM PDT
Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi,Abdallah Bulembo (katikati) akiwasili katika viwanja vya karimjee jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuungana na wasanii kwenye dua maalum ya kuwaombea wasanii waliotangulia mbele ya haki.Kulia ni Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity,Steven Mengele maarufu kama Steve Nyerere.
Msanii wa vichekesho ambaye pia ni muinjilisti kwa sasa Emanuel Mgaya Maarufu kama Masanja Mkandamizaji akiongoza dua kwa upande wa wakristo huku Msanii Jacob Stephen JB akiwa ameishikilia Biblia.Kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Alhaj Mussa Salum ambaye aliongoza dua kwa upande wa waislam,katika shuguli hiyo ya kuwaombea Wasanii waliotangulia mbele ya haki,iliyofanyika jana kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya wadau wa Filamu nchini wakiwa kwenye shughuli hiyo ya kuwaombea Dua Wasanii wote waliotangulia mbele ya haki (waliofariki) iliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar es salaam jana.
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Alhaj Mussa Salum akijadiliana jambo na baadhi ya wadau walioshiriki kwenye dua hiyo.
Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity,Steven Mengele maarufu kama Steve Nyerere akipeana mkono na watu mbali mbali baada ya kumalizika kwa dua ya kuwaombea wasanii waliotangulia mbele ya haki,iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee,Jijini Dar es salaam.
Posted: 17 Aug 2014 01:32 AM PDT
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akizungumza na viongozi wa kanisa Moravian Tanzania wakati akifungua Mkutano wa Kitaifa wa kanisa hilo uliofanyika mwishoni mwa wiki hii mjini Dodoma.
Baadhi ya viongozi wa kanisa la Moravian Tanzania wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa kitaifa wa kanisa hilo hapa nchini uliofanyika mwishoni mwa wiki hii mjini Dodoma.
Posted: 17 Aug 2014 12:01 AM PDT
IMG_0085
Mkurugenzi wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha  Bw Robert Francis  akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo baada ya kufanya hafla fupi iliyofanyika mjengoni kwao ,ya kuwapongeza kwa kushika nafasi ya kwanza katika sekta ya mawasiliano na habari kwa ukanda wa kaskazini maonyesho ya nane nane, Pamoja na  David Rwenyagira aliyepata Tuzo za Tanapa hivi karibuni
IMG_0073
Mkurugenzi wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha  Bw Robert Francis  akiwa anampongeza Mfanyakazi wa kituo hicho David Rwenyagira kwa kupata Tuzo na kushika nafasi ya kwanza upande wa Redio katika eneo la kutangaza utalii wa ndani na mshindi wa pili pekee kundi la kutangaza masuala ya Uhifadhi upande wa Redio zilizotolewa na   Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) hivi karibuni.

Posted: 16 Aug 2014 10:24 PM PDT
Mona Lisa (pia huitwa La Giocconda ambayo kwa Kitaliano ina maana ya furaha au mwanamke mwenye furaha tele) ni mchoro wa mwanzoni mwa karne ya kumi na sita uliochorwa na mchoraji mashuhuri duniaLeonardo da Vinci. Inaaminika kuwa ni mmoja kati ya michoro mashuhuri duniani. Mchoro huu unapatikana katika jumba la maonyesha (makumbusho) la mjini Paris maarufu kama Louvre. Nat King Cole aliutungia wimbo mchoro huu ambao sifa zake si za kawaida
Posted: 16 Aug 2014 09:25 PM PDT
                                                       Na Profesa Mbele
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale. Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katika duka la vitabu la Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 
Kitabu hiki ni mkusanyo wa tenzi tatu za kale maarufu: Fumo Liyongo, uliotungwa na Muhamadi Kijumwa; Al Inkishafi, uliotungwa na Sayyid Abdalla bin Ali; naMwanakupona, uliotungwa na Mwana Kupona binti Mshamu. Kitabu kimehaririwa na M.M. Mulokozi, profesa mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kilichapishwa na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili mwaka 1999.
Hizi ni kati ya tenzi maarufu kabisa katika ki-Swahili. Kwa msingi wa sanaa na maudhui, tenzi hizi zina hadhi kamili ya kuwemo katika orodha ambayo kwa ki-Ingereza huitwa "classics."
Fumo Liyongo ni hadithi inayomhusu shujaa Fumo Liongo, ambaye mimi, kutokana na utafiti wangu wa miaka mingi, napendelea kumwita Liongo Fumo. Huyu ni shujaa wa kale, labda miaka elfu moja iliyopita, na ndiye anayesifika kuliko wote tangu zamani katika jamii ya wa-Swahili.
Alikuwa pandikizi la mtu, mwenye vipaji kadhaa: kuwashinda maadui, shabaha katika kutumia upinde na mshale, ufundi wa kutunga nyimbo na mashairi. Juu ya yote, alikuwa muungwana sana, mfano wa kuigwa. Lakini alifanyiwa visa na ndugu yake ambaye alikuwa mfalme, hadi hatimaye akauawa na kijana mdogo, ambaye alikuwa mpwa wake. 




No comments:

Post a Comment