Yamkini kwasababu ambazo wanazijua
wazazi wako walishindwa kuishi pamoja na kuamua kutengana ukiwa mdogo au wakati
ukiwa na ufahamu halisi, ukajikuta unakua na kulelewa na mzazi mmoja. Labda
hali ya maisha ilikuwa sio mbaya sana kwasababu ya uwezo wa kifedha wa mzazi
uliyebaki naye au labda hali ilikuwa ngumu sana kwasababu ya uchumi mdogo wa
mzazi uliyebaki naye. Yamkini hukupenda hali hii kabisa, ulitamani kukua ukiwa
na wazazi wako wawili, na mara nyingine wala hutaki kukumbuka hali ilivyokuwa
kwasababu inakuumiza. Sijui katika yote hayo umejifunza nini? Natamani liwe
somo litakalokupandia kiu ya kujitunza na kuijenga familia ambayo mtoto/watoto wako
watakua na kulelewa katika familia yenye wazazi wote wawili (baba na mama).
Maumivu na majuto yako yawe wimbo utakao kukumbusha kuwaepusha wanao kupitia
maumivu na majuto uliowahi kuyapitia wewe kwa kutokuzwa na wazazi wawili. Mara
nyingine ni ngumu, ninaelewa, lakini inawezekana – Chris Mauki
KWA WANAUME WALIOKO KWENYE MAHUSIANO
Mambo yanayo kuwezesha kuonyesha penzi kwa mpenzi wako na ambayo yatachochea heshima kutoka kwake – C O U P L E
C – Closeness (Kutamani kuwa karibu naye)
O- Openness (Kupenda kuwa muwazi)
U- Understanding (Kuwa muelewa)
P- Peacemaking (Kuwa mwenye kupenda amani)
L- Loyalty (Kuwa mwaminifu)
E- Esteem (Tambua na onyesha uthamani wa mpenzi wako)

KWA WAKINA DADA MLIOKO KWENYE
MAHUSIANO
Yamkini umeshasikia usemi usemao “mbinu bora ya kuondokana na mwanaume uliyemchoka ni kutafuta mwanaume mwingine” sawa naweza kukubaliana na wewe, lakini jiulize, je kule kuondokana na huyo unayetaka akuache kunakufanya uwe salama na mwenye furaha? Yamkini unaifuata ile methali isemayo “dawa ya moto ni moto” lakini nikutahadharishe tu kwamba sio methali zote zinatenda kazi kwenye mahusiano kama vile zilivyo, ziko nyakati kwenye mahusiano dawa ya kuzima moto siyo kuwasha moto mwingine bali ni kumwaga maji, tena ya baridi kabisa. Usije kuwa na misimamo ambayo itayafanya macho yako yasikauke machozi kwa jinsi utakavyodumu kwenye kulia kwa kuumizwa moyo kila wakati, kwasababu mwisho wa siku utajikuta umekuwa mtaalamu wa kumiliki wanaume wasiokaa. Sasa sijui wote waliopita kwako na ukawaacha uliwapenda? au ndiyo walikuwa wanapita kama wafanyakazi kwenye usahili “interview”! – Chris Mauki

No comments:
Post a Comment